Genesis 14:14-16

14 aAbramu alipopata habari kwamba jamaa yake amechukuliwa mateka, akawaita watu 318 wa nyumbani mwake waliokuwa wamefunzwa kupigana vita, wakawafuatilia hadi Dani. 15 bWakati wa usiku Abramu aliwagawa watu wake katika vikosi ili awashambulie, na akawafuatilia, akawafukuza hadi Hoba, kaskazini ya Dameski. 16 cAkarudisha mali zote, na akamrudisha Lutu jamaa yake na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine.

Copyright information for SwhKC